Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, maandamano haya yalihusisha zaidi ya watu nusu milioni waliokusanyika katika mitaa ya London wakieleza kuwa wanaitaka serikali yao kukomesha ushirikiano wake katika mauaji ya kimbari yanayoendelea dhidi ya watu wasio na hatia wa Gahza, maandamano hayo yalikuwa na sura mbili:
kwanza, kuonesha mshikamano na watu wanyonge wa Ghaza na kutaka mgogoro wa kibinadamu huko umalizike haraka iwezekanavyo; na pili, ilikuwa ni ukumbusho wa kumbukumbu ya miaka 77 tangu kutokea kwa "Yawm al-Nakbah", (siku ya nakbah).
Kadhalika, msemaji wa kampeni ya kuunga mkono Palestina alieleza kuwa maandamano haya yamefanyika kwa lengo la kukumbuka maadhimisho ya mwaka wa 77 tangu kutokea kwa Siku ya Nakbah mwaka 1948. “Tumekusanyika hapa pamoja na tunaiomba serikali yetu isimamishe mara moja ushirikiano wake na watekelezaji wa mauaji ya halaiki,” alisema.
“Nakbah” ni jina ambalo watu wamelipa siku ambayo zaidi ya Wapalestina 750,000 walilazimika kuyaacha makazi yao wakati wa kuundwa kwa utawala bandia wa Kizayuni mwaka 1948.
Maoni yako